Kampuni ya Nyumba za Watumishi (WHC) ni taasisi ya Umma ambayo ilianzishwa mwaka 2013. Kampuni hii inayojihusisha na uendelezaji miliki na usimamizi wa uwekezaji katika miliki.

WHC inatekeleza Mpango wa Taifa wa Makazi kwa Watumishi wa Umma na ina jukumu la kujenga nyumba 50,000 zitakazouzwa kwa mikopo nafuu ya muda mrefu kwa watumishi waishio ndani na nje ya nchi. Mradi huu utakuwa katika awamu tano na utekelezaji wa ujenzi utaanza katika mwaka wa fedha 2014/2015. Kuanzia tarehe 31/07/2017, Serikali imeipa mamlaka WHC kuuza nyumba zake kwa wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Hata hivyo bado Watumishi wa Umma watapewa kipaumbele katika kununua nyumba hasa pindi panapotokea kuna ushindani baina ya wateja katika kupata nyumba husika.

Kama msimamzi wa uwekezaji katika miliki, kampuni hii pia ina jukumu la kusimamia vipande vya uwekezaji katika miliki (REITs). Uwekezaji katika miliki ni aina mpya ya uwekezaji katika Tanzania na uwekezaji huu unatoa fursa lukuki kwa watanzania wote kushiriki na kuboresha kipato chao na kuleta maendeleo ya kiuchumi. WHC inakusudia kufanya kazi na wadau wa ndani na walioko nje ya nchi katika kukuza soko la uwekezaji katika miliki katika namna ambayo kila mtu atanufaika.

WAMILIKI WA WHC

gepfppfnhcnssfnhiflapf

HABARI MPYA

Nafasi za Kazi – Tangazo la Ajira

Waziri wa Ardhi Mh. William Lukuvi atembelea Banda la (WHC) katika Maonesho ya SabaSaba Dar es Salaam

CEO’s Exclusive Interview with Tanzania Invest

ASILIMIA YA MIRADI KUKAMILIKA

WATUMISHI NJEDENGWA ESTATE – DODOMA 45% Kukamilika
BUNJU B HOUSING ESTATE -DAR ES SALAAM 95% imekamilika
MAGOMENI APARTMENTS – DAR ES SALAAM 100% imekamilika
GEZAULOLE RESIDENTS – DAR ES SALAAM 90% imekamilika
KISESA HOUSING ESTATE – MWANZA 100% imekamilika
MKUNDI HOUSING PROJECT – MOROGORO 95% imekamilika